Friday, June 16, 2017

WARSHA YA KARIKACHA & VIBONZO YAMALIZIKA, YAFUNGWA NA BALOZI ARTHUR MATTLI


Balozi na Mwakilishi wa Uswisi Afrika Mashariki, Arthur Mattli, akimkabidhi cheti cha ushiriki wa “Warsha ya Uchoraji Karikacha & Vibonzo,” Saidi Michael maarufu kama “Wakudata” hivi karibuni baada ya kushiriki mafunzo ya kuwajengea uwezo yaliyoendeshwa na asasi ya Nathan Mpangala Foundation (NMF) na kufadhiliwa na ubalozi huo. Katikati ni Mwenyekiti wa NMF, Nathan Mpangala.

Mchora vibonzo Musa Ngarango aka “Masikio Mchongoko,” akilamba ganda lake.

Mchora vibonzo chipukizi, Brenda Kibakaya alidhihirisha kuwa uchoraji vibonzo si kwa wanaume tu.

Magreth Liwembe akimkabidhi zawadi mgeni rasmi Balozi na Mwakilishi wa Uswisi Afrika Mashariki, Arthur Mattli (karikacha cha mke wa balozi iliyonakshiwa kwa saini za washiriki) kwa niaba ya washiriki wenzake.

Mchora vibonzo Simon Regis akitoa neno la shukrani kabla ya kukabidhiwa vyeti.

Baadhi ya karikacha zilizochorwa na washiriki wakati wa mafunzo hayo.

Mwezeshaji na mwenyekiti wa NMF, Nathan Mpangala akiwa na washiriki wakati wa mafunzo karikacha na vibonzo kabla mgeni rasmi hajawasili. Mafunzo hayo ya siku tatu yaliyofanyika jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wachora vibonzo wa “kizazi cha tatu,” yalijikita katika uchoraji karikacha na katuni za maoni unaozingatia misingi.

Picha ya pamoja na mgeni rasmi.
Mchora vibonzo Nestory Fedeliko, akipokea cheti chake.
Maji hufuata mkondo, mchora vibonzo Abdallah Masoud, mdogo wa mchoraji maarufu Masoud Kipanya akipokea cheti chake.
Mchora vibonzo chipukizi, Theresia Kaiza akipokea cheti chake.
Mchora vibonzo Regis Simon naye hakubaki nyuma.
Kwa nini asifurahi! Ndivyo anavyooneka mchora vibonzo Mohamed Jumanne aka "Dr Meddy" wakati akipokea ganda lake.