Sunday, April 16, 2017

MCHORA VIBONZO, NATHAN MPANGALA ALA KIAPO TUZO ZA EJAT 2016

MMOJA wa majaji wa Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) 2016, Nathan Mpangala akiapa mbele ya Jaji Mstaafu, Thomas Mihayo, Dar es Salaam leo huku Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) Bw. Kajubi Mukajanga, akishuhudia. Jopo la majaji litaongozwa na Bi. Valerie Msoka. Majaji wengine ni Bi. Joyce Bazira , Bw. Hassan Mhelela, Bi. Mzuri Issa Ali, Bi. Pili Mtambalike, Bw. Ndimara Tegambwage na Bw. Mwanzo Millinga wakati ambapo jopo la wataalam wa Tuzo ya Maisha ya Mafanikio Katika Uandishi wa Habari 2017 linaundwa na Bi. Lilian Kallaghe ni Bw. Hamis Mzee, Bw. Attilio Tagalile, Bw. Wence Mushi, na Bw. Joseph Kulangwa. Picha: Mwanzo Millinga.