Friday, February 24, 2017

WASANII KUCHORA NA WANANCHI SEHEMU YA WAZI DAR ES SALAAM LEO

KUNDI la wachoraji la '14 voices', la jijini Dar es Salaam, leo litachora litaungana na wananchi katika eneo la wazi iliyopo mtaa wa Samora karibu na mnara wa saa kuchora michoro mbalimbali ili kutoa hamasa kwa Watanzania kuthamini sanaa ya uchoraji. Aidha, malengo mengine ni kushawishi serikali na taasisi zake, mashirika binafsi na mtu mmoja mmoja kupamba ofisi zao kwa michoro ya ukutani kwani huondoa msongo wa mawazo, hufikirisha na pia ni rasilimali. Awali, tukio hilo lilipangwa lifanyike katika bustani iliyopo posta ya zamani lakini kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wao, likahamishwa Samora. Shughuli itaanza saa mbili asubuhi mpaka sita na nusu mchana. Wananchi mbalimbali wameombwa kujitokeza kushiriki. Pichani ni baadhi ya wawakilishi wa kundi hilo.