Saturday, February 25, 2017

WANAFUNZI WAUNGANA NA WACHORAJI KUCHORA MUBASHARA

BAADHI ya wanafunzi waliojitokeza wakifuatilia na kushiriki kuchora wakati kundi la wachoraji la "14 Voices" lilipokuwa likichora mubashara katika bustani iliyo karibu na mnara wa saa katikati ya jiji la Dar es Salaam, jana. Tukio hilo lililenga kuhamasisha taasisi za serikali, taasisi binafsi na jamii kwa ujumla kupamba nyumba zao kwa michoro ya Kitanzania ambayo baadhi ya faida zake ni kupunguza msongo wa mawazo na huvuta muda wa kusubiri huduma kwenye maofisi.