Friday, February 24, 2017

WACHORAJI WACHORA MUBASHARA DAR LEO

WASANII wa michoro ya aina mbalimbali wanaounda kundi la "14 Voices," leo walichora mubashara katika bustani iliyo karibu na mnara wa saa katikati ya jiji la Dar es Salaam. Tukio hilo lililenga kuhamasisha taasisi za serikali, taasisi binafsi na jamii kwa ujumla kupamba nyumba zao kwa michoro ya Kitanzania ambayo baadhi ya faida zake ni kupunguza msongo wa mawazo na huvuta muda wa kusubiri huduma kwenye maofisi.