Monday, February 20, 2017

NYUMBANI kwa Balozi wa Switzerland nchini Tz: Wikendi iliyopita wachoraji 14 toka Tz waliandaliwa mnuso na balozi baada ya kufanya onesho kubwa la michoro nchini Kenya hivi karibuni. Wachoraji hao wamesema wamefanikiwa kufikia malengo waliojiwekea katika onesho hilo na sasa wanajipanga kwa onesho kama hilo litakalofanyika mwisho wa mwaka huu nchini Rwanda. Aidha, ubalozi umepongeza wachoraji hao kwa kujisukuma wenyewe kwa kufanya onesho nje ya mipaka ya Tz.