Thursday, October 13, 2016


ONESHO LA VIBONZO KUFANYIKA MAKUMBUSHO YA TAIFA OKTOBA 20-23, 2016

KAMATI ya "Museum Art Explosion," kesho Ijumaa, tarehe 14.10.2106, saa nne asubuhi itakutana na wachoraji mbalimbali wa vibonzo kuzungumzia onesho la katuni lililoandaliwa na Makumbusho ya Taifa kuanzia tarehe 20-23 Oktoba mwaka huu. Taarifa kutoka katika kamati hiyo inasema, onesho hilo lina malengo ya kuwawezesha washiriki kuonesha na kuuza kazi zao zikiwemo zile zitokanazo na vibonzo mfano posters, fulana nk. Aidha, taarifa hiyo imesema michoro itakayooneshwa si lazima iwe ya kisiasa tu au iliyokwisha toka katika vyombo vya habari, bali hata ambayo haijawahi kutoka alimradi itakuwa imekidhi vigezo itapokelewa. Hii itatoa nafasi hata kwa wale ambao si wachoraji wa kila siku kupata nafasi ya kushiriki. Wachoraji wanahimizwa kushiriki kikao hicho muhimu cha kesho ili wafahamu taratibu za onesho hilo na kupata ufafanuzi pale watakapohitaji. Kwa maelezo zaidi wasiliana na Rais wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi, Adrian Nyangamalle kupitiana namba 0716 124 490. Tafadhali mjulishe na kibonzo mwingine.