Tuesday, October 11, 2016

NATHAN MPANGALA FOUNDATION (NMF) YAMTEMBELEA WAZIRI PROFESA NDALICHAKO

Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako, kifurahia jambo wakati alipokutana na Mwenyekiti wa “Nathan Mpangala Foundation (NMF),” ambaye pia ni mchora vibonzo wa ITV, Nathan Mpangala (katikati) na Mkurugenzi wa “Education Improvement Trust Fund (EITF),” Joseph Chikaka, mjini Dodoma, Jumamosi iliyopita. Ziara hiyo ilitumiwa na NMF kujifunza ili kuona ni maeneo gani programu za NMF zinahusiana na somo la stadi za kazi. NMF ni taasisi isiyokuwa ya kiserikali iliyosajiliwa hivi karibuni ikiwa na malengo kadhaa, moja wapo ni kuwawezesha vijana kujifunza masuala mbalimbali kupitia sanaa za aina mbalimbali. (Picha: NMF)