Monday, October 24, 2016

Ilikuwa ni furaha kwa mtoto Budoya Nyembe (9) baada ya kupata mchoro uliosainiwa na mchoraji vibonzo nchini, Nathan Mpangala hivi karibuni. Kwa kuonesha furaha yake naye akashuka mistari. Budoya anayeishi Dar es Salaam ni mmoja ya watoto wanaofuatilia kwa karibu kibonzo cha Mtukwao kinachorushwa Jumatatu - Ijumaa mara tu baada ya taarifa ya habari ya saa mbili usiku, katika kituo cha ITV.