Tuesday, October 11, 2016

BALOZI wa Tamasha la Majimaji Selebuka, Nathan Mpangala (aliyenyoosha mkono) akitoa mrejesho kuhusu tamasha la Majimaji Selebuka katika mkutano wa wadau uliofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa ‘Nafasi Art Space,’ Mikocheni, jijini Dar es Salaam. Tamasha la Majimaji Selebuka lilifanyika Songea, mkoani Ruvuma mwishoni wa mwezi wa tano mwaka huu. Mbali na heshima hiyo ya ubalozi, Mpangala pia ni mchora vibonzo wa ITV na mwenyekiti wa taasisi ya "Nathan Mpangala Foundation."