Tuesday, October 11, 2016

BAADHI ya majaji wa shindano la Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari (EJAT) 2015, wakifuatilia utoaji tuzo wa shindano hilo lililofanyika katika ukumbi wa Mlimani City, Jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Bw. Nathan Mpangala, Bw. Juma Dihule, Bw. Kiondo Mshana, Bi. Valerie Msoka (Mwenyekiti), Bw. Ndimara Tegambwage na Dkt. Joyce Bazira Ntobi. Kwa mara ya kwanza jopo hilo limemjumuisha mchoraji vibonzo. Mpangala amefanya kazi katika vyombo vya habari kwa zaidi ya miaka kumi. Kwa sasa anachora kibonzo maarufu kwa jina la Mtukwao katika kituo cha ITV. Aidha, ni mwenyekiti wa taasisi ya "Nathan Mpangala Foundation."