Saturday, May 28, 2016

MABALOZI WA TAMASHA LA MAJIMAJI SELEBUKA 2016 TOKA TANZANIA NA MAREKANI WATEMBELEA PERAMIHO JANA.


SALAMU TOKA PERAMIHO, RUVUMA. Balozi wa Tamasha la Majimaji Selebuka 2016 ambaye pia ni mchora vibonzo maarufu nchini, Nathan Mpangala akiwa amekula pozi nje ya kanisa la Mtakatifu Benedict, Peramiho. Balozi huyo alikwenda kutembelea kanisa hilo kubwa lilijengwa na Wajerumani enzi ya ukoloni na mpaka leo bado liko ngangari utafikiri limejendwa jana. Katika tamasha hilo litakalofanyika katika Viwanja vya Mashujaa Songea, linaanza kuunguruma leo ambapo Mpangala atashiriki mbio za kilomita tano na atafundisha vijana na watoto kuchora.
Mabalozi wa Tamasha la Majimaji Selebuka 2016 Anna Schwartz toka Marekani na Nathan Mpangala toka Tanzania katika picha ya pamoja nje ya Kanisa la Mt. Benedict, Peramiho, Ruvuma, jana.
Balozi wa Tamasha la Majimaji Selebuka 2016, Nathan Mpangala toka Tanzania nje ya kanisa la Mtakatifu Benedict, Peramiho, Ruvuma, jana.