Monday, April 04, 2016

KINACHOSABABISHA WATOTO NJITI HIKI HAPA...

Mchora vibonzo Nathan Mpangala, akielezea umuhimu wa matumizi ya vibonzo katika kuuelimisha umma kuhusu suala la watoto njiti wakati wa mkutano wa siku mbili uliofanyika Jijini dar es Salaam hivi karibuni. Katika mkutano huo ulioandaliwa na Doris Mollel Foundation zilielezwa sababu kadhaa zinazosababisha mzazi kujifungua mtoto njiti. Baadhi ni pombe, dawa za kulevya, upungufu wa damu mwilini, uzito mkubwa kwa mama mjamzito, uvutaji sigara/bangi, magonjwa ya kisukari, presha, maambukizi, kifafa cha uzazi, matatizo kwenye cervix inashindwa kujifunga na kujikaza kubeba mtoto, kondo(placenta) inapokuwa na tatizo, kushika mimba haraka baada ya kujifungua mtoto mwingine, mimba ya mapacha, chupa kupasuka kabla ya wakati, msongo wa mawazo, kazi ngumu, vipigo, mimba za utotoni, mimba za uzeeni, kutopata vipimo sahihi na kwa wakati, kutotumia vitamins/foilic acid, lishe na mama mjamzito kutokuhudhuria kliniki. Chukua hatua.