Thursday, March 03, 2016

WATANZANIA WAGUSWA PABAYA, WAUNGANA WATETEA TAIFA LAO

Nathan Mpangala, Dar es Salaam

WATANZANIA watetea Taifa lao! Ndivyo ninavyoweza kusema kufuatia Bi. Rosemary Odinga (binti wa Waziri Mkuu Mstaafu wa Kenya, Bw. Raila Odinga), tarehe 18.8.2015 kuhutubia vijana zaidi ya 1000 huko Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, New York, akidai Bonde la Oltupai maarufu kwa ung’eng’e kama Olduvai Gorge liko Kenya!!!

Mandhari ya Bonde la Olduvai Gorge
Ukurasa huu unakupa maelezo kuhusu urithi huo wa Watanzania. Ni eneo la kiakiolojia linalopatikana Mkoa wa  Arusha, nchini Tanzania, namaanisha Tanzania tu, ambalo ni miongoni mwa maeneo muhimu zaidi duniani. Nasema hivi, Bonde la Olduvai Gorge lipo Tanzania, si Kenya!

Bonde hilo lipo katika Hifadhi ya Ngorongoro na karibu na ile ya Serengeti. Sikia hii, ni mahali ambapo zamadamu (viumbe wa kale waliokaribiana na mwili wa binadamu) waliishi miaka milioni mbili hivi iliyopita. Nasema hivi, Bonde la Olduvai Gorge lipo Tanzania, si Kenya!

Inaaminika zamadamu waliishi katika bonde hilo (kitovu vha binadamu) miaka 17,000 mfululizo. Nasema hivi, Bonde la Olduvai Gorge lipo Tanzania, si Kenya!

Zinjanthropus
Tarehe 17.7.1959, mwanaakiolojia, Mary Leakey aligundua fuvu la kiumbe wa kale. Mary na mumewe wakaliita fuvu hilo Zinjanthropus. Limejaa tele Makumbusho ya Taifa, Dar es Salaam. Nasema hivi, Bonde la Olduvai Gorge lipo Tanzania, si Kenya!

Babu  Zinjanthropus anadhaniwa kuwa mtangulizi wa binadamu wa sasa. Kilomita 45 kusini mwa bonde hilo, kuna eneo linaitwa Laetolia, mwaka 1972 Bi. Leakey aligundua nyayo za kale za zamadamu waliotembea kwa miguu miwili miaka milioni 3.7 iliyopita.  Hilo ndilo Bonde la Olduvai Gorge. Nasema hivi, Bonde la Olduvai Gorge lipo Tanzania, si Kenya! (Chanzo - https://sw.wikipedia.org)