Thursday, March 03, 2016

WANAOISHI KATIKA MAPIPA YA TAKATAKA UINGEREZA WAONGEZEKA

ALIYEKUAMBIA maisha magumu ni Afrika tu nani? Hata nchi zilizotangulia kuna baadhi ya watu moja haikai wala mbili haikai.

Idadi ya watu wasio na makao na ambao sasa wanaishi katika mapipa ya taka inaendelea kuongezeka nchini Uingereza kulingana na kampuni kubwa ya kuzoa takataka nchini humo.

Picha: www.bbc.com/swahili
''Katika barabara unatukanwa na hata kunyanyaswa. Usiku uliopita vijana wachache walikuwa wanatembea karibu yangu na mwengine akanipiga teke la uso. Lakini katika mapipa unaweza kujificha ili watu wasikuone.Kuna joto hakuna mtu anayejua ulipo,''George analezea kuhusu barabara ya Bristol.

Amekuwa bila makao tangu alipopoteza kazi yake ya uhandisi kabla ya krisimasi na kumfanya kushindwa kulipa kodi ya nyumba.

George ni miongoni mwa idadi kubwa ya raia nchini Uingereza aliyepatikana akilala katika mapipa ya takata kulingana na kampuni hiyo ya kuzoa taka ya Biffa.

Mwaka 2014 kampuni hiyo iligundua watu 31 waliokuwa wakilala katika mapipa ya takataka. Mwaka mmoja baadaye idadi hiyo iliongezeka na kufikia 93 na mwaka huu ambao unaisha mwezi Machi, idadi hiyo imefikia 175. 
(Chanzo - http://www.bbc.com/swahili)