Sunday, March 13, 2016

RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI ATEUWA WAKUU WAPYA WA MIKOA, SASA DAR CHINI YA PAUL MAKONDA

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa wakuu wa Mikoa 26 ya Tanzania Bara, ambapo kati yao 13 ni wapya, 7 wamebakizwa katika vituo vyao vya kazi, 5 wamehamishwa vituo vya kazi na 1 amepangiwa Mkoa Mpya wa Songwe.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU, Bw. Gerson Msigwa, imesema uteuzi huo umetangazwa na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Mussa Ibrahim Iyombe leo tarehe 13 Machi, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam.

Mh. Paul Makonda - Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam

Wakuu wa Mikoa walioteuliwa ni kama ifuatavyo; Mh. Paul Makonda - Dar es salaam, Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Elias Kyunga - Geita, Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustafa Kijuu -Kagera, Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga - Katavi, Brigedia Jeneral Mstaafu Emmanuel Maganga - Kigoma na Mh. Godfrey Zambi - Lindi, Dkt. Steven Kebwe - Morogoro.

Wengine ni Kamishna Mstaafu wa Polisi Zerote Steven - Rukwa, Mh. Anna Malecela Kilango - Shinyanga, Mhandisi Methew Mtigumwe - Singida, Mh. Antony Mataka - Simiyu, Mh. Aggrey Mwanri - Tabora, Mh. Martine Shigela - Tanga, Mh. Jordan Mungire Rugimbana - Dodoma, Mh. Said Meck Sadick - Kilimanjaro, Mh. Magesa Mulongo - Mara, Mh. Amos Gabriel Makalla - Mbeya na Mh. John Vianey Mongella - Mwanza.

Pia wamo Mh. Daudi Felix Ntibenda - Arusha, Mh. Amina Juma Masenza - Iringa, Mh. Joel Nkaya Bendera - Manyara, Mh. Halima Omary Dendegu - Mtwara, Dkt. Rehema Nchimbi - Njombe, Mhandisi Evarist Ndikilo - Pwani, Mh. Said Thabit Mwambungu - Ruvuma na Luteni Mstaafu Chiku Galawa - Songwe (Mkoa mpya).

Taarifa hiyo imesema wakuu wa mikoa hao, wataapishwa Jumanne,15 Machi, 2016 saa 3:30 asubuhi Ikulu, Jijini Dar es salaam.