Tuesday, March 29, 2016

"ONGEA NA JANET SHOW " YAMTEMBELEA NATHAN MPANGALA LEO

Mwaandaaji wa "Ongea na Janet Show," Bi. Janet Sosthenes Mwenda akimhoji mchora vibonzo, Nathan Mpangala kuhusiana na nafasi ya wazazi katika kukuza vipaji vya watoto. Mahojiano hayo yalifanyika katika ofisi ya msanii huyo jijini Dar es salaam, leo. Kulia ni mtaalam wa sauti, Bw. Rammy Likote. Usikose kutazama "show" hiyo Alhamis, saa tatu usiku, Clouds Tv.