Saturday, March 05, 2016

MBWANA SAMATTA KUUWASHA MOTO TENA LEO? NI GENK DHIDI YA STANDARD LIEGE

Nathan Mpangala, Dar es Salaam

LIGI ya Ubelgiji, Belgian Pro League inaendelea tena leo kwa michezo kadhaa. Kwa mashabiki wa soka Tanzania na Afrika kwa ujumla watakuwa wanajiuliza, je, Mbwana Samatta ataibeba tena Genk leo? Hapana shaka jibu ni ‘big’ ndio.

Samatta (kushoto) katika moja ya amshaamsha zake Ubelgiji
Baada ya kufunga bao la ushindi katika mechi iliyopita dhidi ya Klabu ngumu ya Club Brugge, mshambuliaji huyo Mtanzania, leo anatarajiwa kuiongoza tena klabu yake dhidi ya wenyeji, Standard Liege, katika mchezo mgumu utaopigwa kwenye uwanja wa Stade Maurice Dufrasne, nchini Ubelgiji. Mara ya timu hizo kukutana, zilitoshana nguvu kwa kutoka sare ya bao 1-1.

Baada ya mtanange wa leo, KRC Genk ambayo kwa mwaka huu kwao ubingwa ushaota mbawa kitambo, itakuwa imebakiza mchezo mmoja dhidi ya KV Oostende utakaopigwa ya Jumapili ya tarehe 13.

KRC Genk iko nafasi ya tano ikiwa ishajikusanyia pointi 45 wakati ambapo Standard Liege wana pointi 38 ikiwa imetulizwa nafasi ya saba. Ukurasa huu unamtakia Samatta kila la kweri katika mchezo wa leo.