Wednesday, February 24, 2016

KWA MWANZO HUU, SAMATTA AANZA VEMA GENK

KUTUA Genk ya Ubelgiji na kuanza kupangwa 'fasta' ni nyota njema kwa straika wa Kitanzania, Mbwana Samatta. Tofauti hali ya hewa, lugha na ukizingatia ndio mara ya kwanza kukipiga Ulaya, baadhi tulitegemea ingemchukua muda kuanza kupangwa. Haikuwa hivyo. Pamoja na kutokea benchi katika mechi zote tatu, ameonekana kuzoea 'mwendo' haraka sana. Hapana shaka ataanza kucheka na nyavu 'vere suni'. Jumapili ijayo, Samatta, wakiwa nafasi ya tano na pointi zao 42, ataiongoza Genk dhidi ya vinara wa ligi Club Brugge yenye pointi 58. Ukurasa huu unakutakia kila la kheri. Kamua baba.

Samatta (77) alipokipiga kwa mara ya kwanza dhidi ya Moeskroen na kuibuka na ushindi wa bao 1 - 0 ugenini.

Samatta (kulia) mawindoni. Hii ilikuwa mara ya pili kuvaa jezi ya Genk na kuinyorosha Beveren bao 6 - 1.

Golikipa na beki wa Lokeren wakitweta baada ya 'amshaamsha' ya Samatta golini kwao.  Gemu hii ya tatu kwa Mtanzania huyo ilimalizika ubao ukisomeka 0 - 0. (Picha: Tovuti ya Genk)