Wednesday, February 24, 2016

HAYA YAKIFANYIKA FANI YA UCHORAJI VIBONZO NCHINI ITAIMARIKA

1. Somo la sanaa lirudishwe mashuleni kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.
2. Mfumo wa ukuzaji vipaji vya sanaa uzingatie uwepo wa fani ya uchoraji vibonzo.
3. Uboreshaji mazingira ya kazi katika vyombo vya habari uhusishe pia jamii ya wachora vibonzo.
4. Kwa kuwa hakuna mfumo rasmi wa ukuzaji uchoraji vibonzo nchini, vyombo vya habari navyo vingaramie mafunzo ya wachora vibonzo.

Nathan Mpangala - Mchora vibonzo

5. Wachora vibonzo tuungane, tupaze sauti ya pamoja kuhusu stahiki zetu ili jamii na mamlaka zinazohusika zifahamu maono na matarajio yetu.
6. Wachora vibonzo tuimarishe vikundi/vyama vyetu ili tuvitumie kutetea stahiki zetu na kizazi kinachokuja.
7. Pawepo na mikataba itakayozingatia mazingira bora ya kazi baina ya wachora vibonzo na vyombo wanavyofanyia kazi.