Saturday, February 27, 2016

GIANNI INFANTINO MAMBO MSWANO, SASA NDIYE BIG BOSS FIFARAIA wa Switzerland, Gianni Infantino, 45, (pichani), ameutwaa Urais wa Shirikisho la Soka Duniani, FIFA nafasi iliyokuwa chini ya Sepp Blatter kwa miaka 18 katika uchaguzi uliofanyika katika Jiji la Zurich, jana.

Katibu huyo Mkuu wa UEFA toka 2009 ambaye pia ni mwanasheria, alijizolea kura 115 kati ya 207 katika raundi ya pili na kumtuliza mpinzani wake, Sheikh Salman al-Khalifa wa Bahrain.

Mfanyabiashara wa Afrika Kusini, Tokyo Sexwale, maji yalizidi unga mapema, akaingia mitini kabla ya kura kuanza kupigwa.


Katika raundi ya kwanza, Infantino aliduwazwa baada ya kupata kura 88, Sheikh Salman 85, Mwanamfalme Ali 27 na Champagne 7.

Baadhi ya ahadi za Infantino; atairudisha FIFA katika ubora wake, ataongeza idadi ya timu zinazoshiriki kombe la dunia toka 32 mpaka 40 na atamwaga mapesa mengi zaidi ya maendeleo ya soka kwa nchi zote. (Chanzo: Tovuti mbalimbali)