Thursday, February 25, 2016

MMOJA WA WAGENI WALIOALIKWA KWENYE MKASI 2015 ALIKUWA MCHORA VIBONZO NATHAN MPANGALA

MCHORAJI vibonzo maarufu nchini, Nathan Mpangala (kulia) amewashukuru waandaaji wa kipindi cha Mkasi kinachorushwa katika Kituo cha EATV kwa kutoa nafasi kwa watu mbalimbali bila kujali uwezo ama sekta watokako.

Mpangala alisema Mkasi wamealika wageni wa aina mbalimbali jambo ambalo ni zuri. Nashauri waendelee kutupia jicho zaidi sanaa za ufundi. Huko kuna wasanii na hadithi zao nyingi na nzuri ambazo bado hazijasimuliwa.