Friday, August 29, 2014

WASANII WASEMA WATAPAMBANA MPAKA HOJA ZAO ZIJUMUISHWE KATIKA KATIBA MPYA


Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mh. Samuel Sitta (kulia), akisisitiza jambo kwa wawakilishi wa mashirikisho ya sanaa mjini Dodoma hivi karibuni. Mashirikisho hayo yamekuwa yakipambana kufa na kupona kuhakikisha katiba mpya inatambue wasanii kama kundi maalum na pia ilinde mali zisizoshikika yaani miliki bunifu (intellectual property). Maoni ya mashirikisho hayo yalishatolewa katika hatua za awali za utoaji maoni na pia kupitia mabaraza lakini kwa bahati mbaya, hayakujumuishwa katika rasimu. Waliokaa kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanamuziki Tanzania, Bw. John Kitime, Rais wa Shirikisho la Filamu, Bw. Simon Mwakifwamba na Makamu mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Bi. Samia Suluhu Hassan. (Picha zote kwa hisani ya ofisi ya Bunge la Katiba).

Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mh. Samuel Sitta (kushoto), akipata sababu za kina kwa nini wasanii wanataka katiba mpya itambue kuwa wasanii ni kundi maalum na pia ilinde mali isiyoshikika au kwa lugha nyepesi miliki bunifu (intellectual property).

Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mh. Samuel Sitta akikabidhiwa nyaraka yenye hoja ya uzengezi (lobbying) kutoka kwa kiongozi wa msafara wa mashirikisho ya sanaa Tanzania ambaye pia ni Rais wa Shirikisho la Filamu nchini, Bw. Simon Mwakifamba, mjini Dodoma hivi karibuni.

Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mh. Samuel Sitta katika picha ya pamoja na wawakilishi wa mashirikisho ya sanaa nchini. Kulia kwake ni makamu wake Bi. Samia Suluhu Hassan.

Makamu Mwenyekiti  wa Kamati namba tano ya Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Assumpter Mshama, akishibishwa hoja za kina kwa nini wasanii wanataka katiba mpya itambue wasanii kuwa kundi maalum na pia ilinde mali isiyoshikika au kwa lugha nyepesi miliki bunifu (intellectual property) toka kwa Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanamuziki Tanzania, Bw. John Kitime, mjini Dodoma hivi karibuni.
Mjumbe wa Kamati namba moja ambaye pia ni Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda (aliyetupia koti), akiteta jambo na baadhi ya wawakilishi wa mashirikisho ya sanaa za nchini waliokwenda Bungeni kufanya uzengezi (lobbying) hivi karibuni. Kushoto kwa Waziri Mkuu ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Ummy Ally Mwalimu.
Wawakilishi wa mashirikisho ya sanaa nchini katika picha ya pamoja na Kamati namba tisa.
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mh. Samuel Sitta (kulia) na nguli wa muziki nchini, Bw. Abdul Salvador, wanaonekana wamekumbuka enzi zileee. Walikutana katika viwanja vya Bunge maalum la Katiba mjini Dodoma hivi karibuni. Wengine kutoka kushoto ni Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania Bi. Stara Thomas na Mwakilishi wa Shirikisho la sanaa za ufundi na mchora vibonzo ITV, Bw. Nathan Mpangala.

Mjumbe wa Kamati namba tisa ambaye pia ni mwakilishi wa wasanii kwenye Bunge la Katiba, Bw. Paul Mtenda (katikati) akifurahia jambo na baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo wakati ujumbe wa mashirikisho ya sanaa nchini, ulipotembelea kamati hiyo hivi karibuni mjini Dodoma.

Sehemu ya wasanii wanaharakati waliotembelea Bunge Maalum la Katiba hivi karibuni ili kuhakikisha katiba mpya inatambua wasanii kuwa kundi maalum na pia ilinde mali isiyoshikika au kwa lugha nyepesi miliki bunifu (intellectual property). Mwenye shati rangi ya bahari ni mjumbe kamati namba tano, Mh. Paul makonda.

Baadhi ya wasanii waliotembelea Bunge Maalum la Katiba hivi karibuni wakifuatilia hoja zao.

Wasanii wapiganaji wakitafakari mustakhabari wa taaluma yao kama katiba mpya haitatambua upekee wao na ulinzi wa mali isiyoshikika kwa lugha rahisi miliki bunifu (intellectual property), mjini Dodoma hivi karibuni.