Monday, August 26, 2013

WAFANYE WATABASAMU YATABASAMU NA WATOTO HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI

Mratibu wa mradi wa kujitolea wa Wafanye Watabasamu, Katunisti Nathan Mpangala ‘Kijasti’ (mwenye kijibegi mgongoni), akisaidiana na familia, ndugu, jamaa na marafiki kuteremsha zawadi kwa ajili ya watoto wanaoumwa saratani, Jumamosi iliyopita, Hospitali ya Taifa Muhimbili.  Karibu na ‘Kijasti’ kulia ni ‘Mama Kijasti’. Photo: Masoud Junior

Wachora vibonzo, Nathan Mpangala ‘Mtukwao’ wa ITV, (kulia) na Abdul King O ‘Kaboka Mchizi’ wa Nipashe, wakichora na malaika wanaoendelea na matibabu ya saratani katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, jijini Dar es Salaam, Jumamosi iliyopita, wakati wa ziara ya mradi wa Wafanye Watabasamu, hospitalini hapo. Photo: Masoud Junior

Baadhi ya watoto wanaotibiwa saratani, Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam, wakionesha uhodari wa kuchora wakati walipotembelewa na mradi wa Wafanye Watabasamu, unaoratibiwa na Nathan Mpangala, Jumamosi iliyopita. Watoto hao wapatao 80, walizawadiwa sabuni za kuogea/kufulia, dawa za meno, biskuti, toilet papers, mafuta ya kupakaa, matunda na vifaa mbalimbali vya kuchorea toka kwa marafiki wa mradi huo. Photo: Godfrey mambo

Vipaji vilisheheni. Wafanye Watabasamu inawaombea mpate nafuu ya mapema ili mkakuze vipaji vyenu. Photo: Masoud Junior