Tuesday, August 27, 2013

MARAFIKI WA WAFANYE WATABASAMU WACHORA NA WATOTO TULIOLAZWA MUHIMBILI

DAH, SIKU NYINGI SIJACHORA! Mmoja wa watoto wanaendelea na matibabu Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam, akiwa bize na rangi wakati walipotembelewa na mchora katuni Nathan Mpangala kupitia mradi wake wa kujitolea wa Wafanye Watabasamu, Jumamosi iliyopita. Mradi huo unaoshirikisha ndugu, jamaa, marafiki na wachoraji wenzake, ulikwenda kuwafariji kwa kuwapa zawadi kisha kuchora nao.

Mratibu wa mradi wa kujitolea wa Wafanye Watabasamu, Katunisti Nathan Mpangala ‘Mtukwao’, akishea jambo na mmoja wa malaika Hospitali ya Taifa Muhimbili, upande wa saratani, Jumammosi iliyopita.

KUCHORA TU, HAPA MMEFIKA! Pamoja na maumivu ya saratani aliyonayo, bado aliweza kuthibitisha kuwa anaweza.

HEBU NIJIACHIE MIE. Ama hakika linapokuja suala la kuchora, hakuna mtoto anayekataa.

Marafiki wa Wafanye Watabasamu, walionesha tabasamu mapemaaaaa.

NIPO BIZE. Sanaa ina mchango mkubwa katika kupunguza msongo wa mawazo na kusahaulisha maumivu.

HUWA NACHORA HIVI… Mchora vibonzo wa ITV ambaye pia ni mratibu wa Wafanye Watabasamu, Nathan Mpangala akiwa na mchora vibonzo wa baadae.

NYUMBA TU, SIMPO. Akiendelezwa atakuja kuwa mchoraji mahiri wa majengo.

Mchoraji katuni wa gazeti la Nipashe, Abdul King O aka ‘Kaboka mchizi’, aliungana na Wafanye Watabasamu kuwatabasamisha malaika hawa.

Mchora katuni Adam Lutta aka Baba Tau, alikuwa miongoni mwa Wana-Wafanye Watabasamu.

KAZI IMETULIA.