Monday, May 14, 2012

WAMAREKANI WADAI KUGUNDUA KINGA YA VIRUSI VYA UKIMWI

Kinga ya virusi vya HIV
AINA moja ya dawa iliyothibitishwa kuwa na uwezo wa kuzuia maambukizi ya virusi vya HIV imepiga hatua muhimu ya kukubalika kutumika nchini Marekani.

Jopo la washauri wa Serikali ya Marekani wameidhinisha matumizi ya dawa aina ya Trevada kwa watu walio katika hatari kubwa ya maambukizi ya virusi vya HIV ambavyo huvuruga kinga ya mwili.

Dawa hiyo Truvada, imekuwa ikitumiwa na watu wanaoishi na virusi vya ukimwi nchini Marekani tangu mwaka wa 2004. Utafiti umeonyesha kuwa dawa hiyo inaweza kuwakinga watu wasiokuwa na virusi dhidi ya maambukizi.