Thursday, May 03, 2012

UMESHAWAHI SIKIA HII?


TAFITI zinaonesha kuwa, paka akiporomoka toka ghorofa ya tatu ana nafasi ndogo ya kupona tofauti na akidondoka toka ghorofa ya ishirini. Inasemekana wakati akiporomoka, humchukua mpaka ghorofa nane kujitambua kuwa yuko kwenye msala. Hivyo kwa jengo la zaidi ya ghorofa nane huumpa nyau nafasi ya kujipanga wakati akiwa hewani hivyo hukutua chini kiulaini. Na ikitokea kapuruchuka toka ghorofa ya tatu, akifika chini ni chapati!!