Wednesday, May 02, 2012

TUME YA KURATIBU MAONI YA KATIBA MPYA YAKABIDHIWA OFISI KATIKA JENGO JIPYA LA WIZARA YA MAMBO YA NDANI


Katibu Mkuu kiongozi, Balozi Ombeni Sefue (kushoto), akimueleza jambo  Mwenyekiti wa Tume ya kuratibu maoni ya Katiba mpya, Waziri mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba wakati wa makabidhiano ya  ofisi ya Tume hiyo iliyopo katika jengo jipya la Wizara ya Mambo ya Ndani, ghorofa ya kwanza, Jijini Dar es Salaa. Aliyevaa suti nyeusi ni Waziri wa Sheria, Mh. Celina Kombani na kushoto kwake ni mbunge wa CCM viti maalum, Bi. Angela Kairuki. [Picha: Blogu ya Fullshangwe]

Katibu Mkuu kiongozi, Balozi Ombeni Sefue (kushoto), akimtembeza Mwenyekiti wa Tume ya kuratibu maoni ya Katiba mpya, Waziri mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba  katika ofisi mpya ya Tume hiyo iliyopo katika jengo jipya la Wizara ya Mambo ya Ndani, ghorofa ya kwanza, katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika leo kwenye jengo hilo, jijini Dar es salaam. Katikati ni Waziri wa Sheria na Katiba, Mh. Celina Kombani. [Picha: Blogu ya Fullshangwe]