Friday, May 04, 2012

SIMBA YATWAA UBINGWA 2012 IKIWA MASKANI

MNYAMA leo kaanza kula shushu na kushangilia ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya Azam FC kulambwa  mabao 2-1 na Mtibwa Sukari kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Simba iliyobakiza mechi moja na mtani wake wa jadi, Yanga, imeshatia kibindoni pointi zake 59 safi, ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote msimu.
Wakata miwa

Kwa matokeo ya leo, Wanalambalamba, Azam wametulizwa nafasi ya pili ambapo watashiriki Kombe la Shirikisho la Soka Afrika mwakani.

Wanajangwani wao mwaka huu wamevuna mabua kwani hata kama Jumapili wakiichapa Simba watabaki nafasi ya tatu.

Katika mchezo wa leo, hadi mapumziko, tayari Mtibwa walikuwa wanaongoza kwa bao 1-0 lililowekwa kimiani na Awadh Issa dakika ya 25, akiunganisha kona iliyochongwa na nyota wa gemu ya leo, Juma Abdul.
Machampioni, SSC

Wakipewa tafu ya nguvu na mashabiki wa Msimbazi, Wakatamiwa toka Manungu, wakacheka na nyavu tena dakika ya 59, mfungaji akiwa ni Juma Abdul.

Wanalambalamb walipata bao la kufutia machozi katika dakika ya 62 kupitia kwa John Bocco.