Sunday, May 06, 2012

SIMBA, YANGA HAPATOSHI TAIFA LEO

Na Ripoti Wetu, Dar
Wakongwe wa soka nchini, Simba na Yanga, leo watapepetana katika mchezo wa kufunga pazia la Ligi ya Kuu Bara, utakaochezwa kwenye kiota maridadi cha Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Wana-Msimbazi
Gemu hii inachukuliwa ni ya kulinda heshima kwani tayari Wana-Msimbazi washajitangazia uchampioni wa mwaka huu kwa kufikisha pointi 59 ambazo piga uwa haziwezi kufikiwa na timu yeyote.

Historia inaonesha kuwa, wakutanapo wakongwe hawa, nyasi huumia sana kwani hata kama timu moja inakuwa dhaifu au imezongwa na migogoro, hujitutumua na hupigana kufa na kupona kuhakikisha inasuuza nyoyo za mashabiki wao.

Wana-Jangwani
Simba iliyojichimbia Zenji, itategemea silaha zake kama Juma Kaseja, Emmanuel Okwi, Haruna Moshi ‘Boban’, Felix Sunzu, Juma Nyoso, Kelvin Yondan na Kapombe.

Nao Yanga iliyokuwa Bagamoyo, hapana shaka itawategemea Felix Kiiza, Yew Berko, Haruna Nyoinzima, Nsajigwa ‘Fusso’ na Jerry Tegete.