Thursday, May 10, 2012

MICHUANO YA NETIBOLI AFRIKA: TAIFA QUEENS YAIBURUZA ZAMBIA LEO

TUMESHINDA. Wachezaji wa timu ya Taifa ya Netiboli, Taifa Queens, wakipongezana baada ya kuichapa Zambia magoli 37-33 leo asubuhi, katika michuano ya Ligi ya Netiboli ya Afrika inayoendelea katika Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es Salaam.
Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Netiboli, M.Hassan(GS), akijiandaa kutumbukiza mpira.
Sehemu ya umati wa Watanzania uliojitokeza leo asubuhi katika Uwanja wa Taifa kuipa shavu Timu ya Taifa ya Netiboli ya Tanzania wakati ilipokuwa ikicheza na Zambia. Taifa Queens iliibuka na ushindi wa magoli 37-33.
Mchezaji wa Zambia, Mukamba(WD), akigalagala kufuatia mchakamchaka toka kwa wachezaji wa Timu ya Taifa ya Netiboli leo asubuhi katika michuano ya Netiboli ya Afrika inayoendelea Jijini Dar es Salaam. Tanzania iliibuka na ushindi wa magoli 37-33.