Sunday, May 06, 2012

MCHIZI BALOTELI ACHAFUA HALI YA HEWA TENA, AJIRUSHA NA VIMWANA USIKU KUCHA

Manchester, Uingereza

Wakati kiboko ya Man U, Mancester City inashuka uwanjani kuumana na New castle leo, mshambuliaji hatari, Mario Baloteli, usiku wa kuamkia alhamisi, alionekana akitumbua raha maskani kwake huku akiliwazwa na warembo wanne aliowakodi toka kampuni ya McKenzies Escort agency ya Uingereza.

Nyota huyo mtukutu wa Kitaliano, aliwalipa wanawake hao na kujirusha nao usiku wa kuamkia alhamisi. Vyanzo vya habari vinadai, marafiki zake waliondoka nyumbani kwake saa 11.45 asubuhi – saa chache kabda hajajitupa mazoezini.

Mario Baliteli
 ‘Wasichana walionekana wako bwii. Habari ya pati hii itawashitua wapenzi wa Mancheter City ukizingatia leo wanashuka dimbani kukabiliana na timu isiyotabirika ya New Castle, mechi ambayo itawawezesha kunyemelea ubingwa wa Ligi Kuu’, majirani waliuambia mtandao wa The Sun.
 
Balotelli, 21, alialika vimwana hivyo baada ya kutemwa na kifaa chake, mwanamitindo, Raffaella Fico, 23. Inadaiwa alitemwa baada ya mtukutu huyo kuwa na uhusian ana vichenchede wengine.

Ili kuhakikisha usiku unakuwa mtamu na wa pekee, Mario aliwakamatisha mshiko wa paundi 245 kila mrembo.

Mchizi Mario akijiachia
Chanzo cha habari hii kinasema, kampuni hiyo ilituma warembo wanne kwenda kula raha kwa Mario usiku huo. Madada hao walijirusha mbaya na mchizi huyo ambaye alikuwa na washikaji wake. Kawaida vimwana hao hufanya kazi mpaka saa nane usiku, lakini usiku huo walipitiliza wakidai kuwa waliamua kuendelea kupare na mshikaji kwa sababu ni mteja maarufu.

Binti mmoja aliondoka saa 11 asubuhi lakini wengine waliendea kula raha huku wakiimba. ‘Mario ana sehemu ya kuogelea na aliandaa shampeini za kumwaga, nina hakika walikula gudi taimu’ alidai jirani mmoja.

Hata hivyo, pamoja na kujirusha usiku kucha, Balotelli akiwa kwenye Range Rover yenye thamani ya paundi 60,000 akatokeza mazoezini. 

Akijongea mazoezini
 Kama haitoshi, usiku wa Alhamisi, akajitupa tena klabu ya usiku ya kushuhudia tuzo ya mchezaji bora wa mwaka. Mitaliano huyo mwenye thamani ya paundi milioni 24, amekuwa mchezaji wa pili kuripotiwa kukodi mabinti toka McKenzies. 

Mwaka 2007 akiwa Manchesetr United, mshambiliaji hatari wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo, aliwahi kualika wasichana watano nyumbani kwake.