Monday, May 07, 2012

MAFUNZO NA TAARIFA ZA MARA KWA MARA KWA WACHORA KATUNI ZA MAONI NI MUHIMU

MEI 3 kila mwaka, vyombo vya habari duniani, husheherekea Siku wa Uhuru wa Vyomo vya Habari Duniani. Wakiwa sehemu ya wana habari, wachora katuni wametoa mchango mkubwa nchini kwenye upasishanaji habari. 

Kumekuwa na changamoto nyingi zinazoikabili jamii hii, kubwa ni mazingira mabovu ya kazi, malipo duni, na ukosefu wa mafunzo ya mara kwa mara.

Wachoraji katuni wanahitaji mafunzo ya mara kwa mara yatakayosaidia kuongeza uweledi katika kazi zao za kila siku. 

Natoa wito kwa taasisi za serikali, makampuni, asasi zisizo za kiserikali na wadau wengine kuhakikisha wanawajaza taarifa za shughuli zao wachoraji katuni ili inapotokea kuchora masuala yanayohusu sekta zao basi wachore kwa usahihi. 

Nazishukuru taasisi zote ambazo zimekuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanatoa mafunzo kwa wataalamu hawa wa katuni. 
MAFUNZO: Mkurugenzi Mkuu, Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), Bw. Emmanuel Humba (katikati) akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina kwa wapigapicha na wachora katuni iliyofanyika jijini Dar ers Salaam mwaka 2010. Kushoto ni Mkurugenzi wa wanachama na Uendeshaji wa NHIF, Hamisi Mdee na Katunisti, Nathan Mpangala. Mfunzo ya aina hii ni muhimu kwa wachora katuni.