- Mwanamke,60, atiwa meno na duma kwa dakika tatu, mumewe atimua, apozi sehemu kuchukua picha za tukio
- Ana bahati hajapoteza jicho, wasema madaktari
- Meneja wa sehemu hiyo awatetea duma, asema walijua ni mida michezo.
![]() |
Bi. Violet D'Mello, sekunde chache kabla hajaonjweshwa shubiri. |
Bi.Violet D'Mello, 60, alikuwa akigalagazwa
vumbini na duma mkubwa baada ya kuingia kwenda kuingia eneo lililohifadhiwa wanyama
pori ambapo watalii huja kupiga picha na wanyama hao.
Mama huyo wa miaka 60 toka Uingereza, alikuwa
holidei na laazizi wake Bw. Archie, 64, wakati alipopata suluba hiyo mara alipojikuta chini huku duma wakimtafuna
kichwani, tumboni na miguuni.
Bi. Violet, ambaye mara baada ya tukio
alikimbizwa hospitalini anasema shughuli ilikuwa hevi na ilitokea fasta. ‘Ghafla nikajikuta nimewekwa kati, mara
wakaanza kunitafuna kichwani’, alisema.
‘Nilirushwa ardhini, nikazuga kama nimekufa. ‘Wanaume’
wakaendelea kunitia meno miguuni vizuri tu.’
Mmoja wa walinzi wa eneo hilo alifanikiwa
kumtimua duma mmoja kutoka kwa Bi. Violet, wakati anahangaika na mwingine, mara
aliyetimuliwa akajumuika tena kwenye gemu. Wakamtupa tena chini mama huyo na
kuendelea kuigombea miguu yake kwa hari, kasi na nguvu zaidi.
Kundi la watalii likajitokeza na kuwavuta
duma, Bi. Violet akapata upenyo, pamoja
na kuwa na mwili mkubwa, Bi. Vai alikuwa mwepesi kama kishada, akamwaga mbio na kupenya kwenye kageti kadogo.
Jambo la kushangaza, mume wa Bi. Violet, Bw.
Archibald, msala ulipoanza tu akala kona, akaenda kusimama sehemu na kuanza
kuchukua snepu za tunda lake wakati linagalagazwa.
Baada ya kashikashi, meneja wa mahala hapo, Mike
Cantor alimkimbiza Bi. Vailet hospitalini ambako alishonwa nyuzi kadhaa kichwani na kutibiwa
majeraha karibu na jicho na mguuni.
![]() | |
Hatari: Duma akitafiti ili kujua kama Bi. Violet analika |
Jana(juzi), Bi. Vailet aliliambia gazti la
Herald la Sauzi kwamba, lilikuwa ni tukio la dakika chache lakini lilitisha. 'Walikuwa wanaonekana kama wamepagawa. Wenye
shauku na ghafla hali ya hewa ikachenji tena haraka sana. Holidei ikageuka kuwa
kizaazaa', alidai Bi Vai.
Mtaalamu wa wanyama wakali, Bw. Graham Kerley,
toka Centre for African Conservation Ecology, amewataadharisha watalii kuwa
duma ni hatari zaidi kwa watoto kuliko watu wazima, amewashauri wazazi kutosogeza
watoto karibu na mnyama huyo.
Mkasa wa Bi. Violet umetokea hivi karibuni wakati
walipokuwa wanakula holidei yao sehemu ya kuhifadhia wanyama pori ya Kragga
Kamma karibu na mji wa Port Elizabeth huko kwa Mzee Madiba.
![]() |
Bi.Violet akiwa taabani huku ‘vidume’ vikijadiliana jinsi ya kuanza shambulizi lingine |
Bw. D'Mello, mume wa Bi. Violet, ambaye
alikula kona wakati wa mshikemshike, ameelezea kilichowatokea baada ya kulipa
randi 50 ili wakawaone duma kwa ukaribu.
Anasema: Tulifika mahala hapo na kulikuwa na
duma wawili. Kulikuwa na ubao wa matangazo ukisomeka; 'unaweza kuwasogelea
wanyama hao kwa msaada wa wafanyakazi wa eneo hilo.'
‘Tuliona poa, tukaamua kuwasogelea, duma
walikuwa wametulia. Mbali na sisi kulikuwa na familia nyingine yenye mtoto’, alisema Bi Vai.
‘Msindikizaji wetu alikuwa mwanamke,
alituambia tunaweza kuwasogelea duma na kuwagusa kiulaini tu. Lakini mama
watoto alipowasogelea, duma wale wakaondoka’, aliongeza kusema.
‘Msindikizaje akasema, saa hizi watakuwa
wamechoshwa na umati wa watu. Tukaona tuondoke, kabla hata hatujapiga hatua mbili
mara duma mmoja akamng’ang’ania mtoto wa kike wa ile familia tuliyokutana nayo
pale.
‘Alilia kwa nguvu, tukarudi kujua
kulikoni. Mtoto alikuwa ameangukia tumbo lake na duma alikuwa akimng’ata paja’
![]() |
Shambuli lilichukua karibu dakika tatu na mume ndiye aliyekuwa akikung’uka picha zote hizi! |
'Dume wote walikuwa wanashughulika na mimi
sikuwa na la kufanya. Wana kucha kali na walikuwa wana ubavu ajabu’, alidai mama huyo.
.
Cha uwoga, Mr D'Mello, mume wa Bi. Violet, ambaye alikuwa anagonga picha wakati mkewe anashughulikiwa na duma, alisimulia jinsi duma walivyotia jaka moyo na kumfanya atimue mbio na kubaki hajijui akimtazama mai waifu wake akiogelea vumbini.
Cha uwoga, Mr D'Mello, mume wa Bi. Violet, ambaye alikuwa anagonga picha wakati mkewe anashughulikiwa na duma, alisimulia jinsi duma walivyotia jaka moyo na kumfanya atimue mbio na kubaki hajijui akimtazama mai waifu wake akiogelea vumbini.
Alisema: ‘Lilikuwa jambo la ajabu, kuogofya
na kuchanganya. Mai waifu wangu alikuwa vumbini na duma
alikuwa akimtia meno kichwani na mapajani huku duma mwingine akimkwaruza.’
‘Sikuwa na la kufanya, isitoshe msindikizaji
wetu hakuwa hata na bakora ya kujilinda yeye mwenyewe. Nikaona cha kufia nini,
nikala kona’
Alisema: ‘Baadae mama mmoja wa mapokezi
alisikia kelele akaja na kiboko ambacho msindikizaji wetu alikitumia kuwatishia
duma wale.’
![]() |
Duma kazini |
Meneja wa hifadhi ya Kragga Kamma park, Bw.
Mike Cantor, aliliambia Herald kwamba hawajui nini kiliwatia upepo duma mpaka
wakashambulia watalii. Alisema duma hao wa tumbo moja, wanaoitwa Mark na Monty,
wametunzwa na wao toka walipozaliwa na wamepoteza kabisa tabia za wanyama pori.
Kragga Kamma game park ni sehemu ya mtu
binafsi huko Sauzi, iliyo katika makazi ya watu ambako pamehifadhiwa wanyama kama nyati,
twiga, pundamilia na duma. [Chanzo: Mashirika]