Thursday, May 03, 2012

DARASA MUHIMU KWA WATUMIAJI WA MITANDAO

JINSI UNAVYOACHA TAARIFA ZAKO KWENYE MITANDAO


Kila unapotembelea kurasa Fulani kwenye mtandao kuna taarifa Fulani
unaziacha labda kwenye tarakishi uliyotumia , kivinjari ulichotumia
kutembelea kurasa hizo za tovuti au huduma uliyotumia kwa ajili ya
kujiunganisha na mtandao .

VITU VYA MUHIMU
Fungua Kivinjari chako ( Browser ) Bonyeza CTRL shikilia chini bonyeza
H Historia ya Kurasa zilizotembelewa na muda itajileta .

UKITAKA KUFUTA
Bonyeza CTRL + Shift + DEL
Kila Kivinjari ( Browser ) kinaweza kuwa na njia tofauti lakini vingi
ni sawa tofauti ni lugha inayotumika

TAARIFA ZAKO ZINAVYOKUSANYWA  .
Watu wengi wageni haswa wale wanaojifunza jinsi ya kutumia mtandao
( internet ) huacha taarifa zao kwenye mitandao mbalimbali pasipo
kujua kwa kujaza fomu mbalimbali , kujiunga kwenye mitandao jamii .

Tovuti zenye vitubwasha vya Huduma mbalimbali ( Buttons ) zinazoweza
kukuunganisha na mitandao mengine kama ya Facebook , Yahoo , Google ,
Ukifungua kwa mfano www.yahoo.com utakuta button ya Facebook ukigonga
kidubwasha hicho taarifa zako zinaweza kuchukuliwa na kuhifadhiwa kwa
ajili ya shuguli nyingine .

HUDUMA ZA BURE
Unapojisajili na huduma za barua pepe za Bure kama Gmail , Yahoo ,au
Hotmail unaweza kukutana na huduma ya History ambayo huweza kuhifadhi
vile vyote unavyotafuta kwa njia ya mtandao kutumia search engine
mbalimbali kama ni google au yahoo , ingawa unaweza kuzima huduma hii
lakini kwa nyuma huduma hii inaweza kutumika bila ya wewe kujijua .
Hukatazwi kutumia huduma za Bure kwenye mitandao lakini unapotumia
hizi za bure kuna baadhi ya vitu utashindwa kufanya kwa mfano kuondoa
matangazo , kuwa na nafasi kubwa ya kuhifadhia vitu vyako , kuangalia
vitu vyako popote ulipo au hata kualika wengine .

MITANDAO YA KIJAMII NA MARAFIKI
Pale unapojiunga na mitandao ya kijamii inayoruhusu kuweka taarifa
binafsi kama picha , kualika marafiki na  mambo mengine hapo utakuwa
umetengeneza njia nyingine ambayo taarifa zako ni ngumu kupotea .

Mitandao mingi ya kijamii kama Facebook na Hi5 imeweka taratibu za
kuficha baadhi ya taarifa kwa ajili ya watu Fulani tu lakini haijaweka
wazi kuhusu matumizi ya taarifa kwa kampuni haswa za matangazo .

MATUMIZI YA TAARIFA ZINAZOKUSANYWA
Taarifa zako zinaweza kutumika kwenye matangazo au mawasiliano mengine
lakini zaidi ni matangazo pale unapopata matangazo zaidi ya 100 kwa
siku moja kwenye email yako , kama ni simu ya mkononi pia ni hivyo
hivyo utaweza kupokea sms nyingi za matangazo na offer mbalimbali .

Kabla hujajaza fomu au kujiunga na huduma hizi ni vizuri usome Privacy
Policy ya Tovuti husika .

TARATIBU ZA KUFUTA TAARIFA ZAKO
Tovuti nyingi zina taratibu zake za kufuta taarifa kwenye database zao
lakini nyingi zinategemeana na sheria za nchi husika kuhusu Ulinzi na
usalama wa Taarifa Binafsi za watu , katika tovuti nyingi kama yahoo ,
wanachukuwa miezi 6 ili kufuata email yako na taarifa zake kabisa ,
katika google wanaweza kufuta hapo hapo ila hawasemi kama kuna
taratibu nyingine wanazifuata baadaye .

Kutokana na uhalifu kukuwa na vitendo vya ugaidi ufutaji wa taarifa
kwenye mitandao imekuwa unachelewa mpaka pale itakapodhibitika kwamba
anuani zako ni salama .

NENO LA MWISHO
Kuacha taarifa zako kwa njia ya mtandao kuna kuweza kuwa na manufaa
haswa pale unapojua kile unachofanya na umesoma masharti vizuri ya
tovuti husika maana kama ni za nafasi za kazi wanaweza kukuandikia
barua na kukujulisha , kama ni masuala ya taaluma watu wanaweza kusoma
tafiti zako na michango mengine nao wanaweza kuchangia .
Muhimu ni kujua Taarifa zako zinavyotumika kwenye mitandao haswa ya
Kijamii .
[Chanzo:  YONA FARES MARO, Wanabidii}
+255786 806028