Friday, May 04, 2012

CHADEMA WAIGWAYA KEKI YA SHY ROSE BANJI

WABUNGE wa Bunge la Jamhuri ya Muungano kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi waliangua vicheko pale wenzao wa CHADEMA walipoikwepa kuigusa na kuila keki ya birthday ya Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Bi. Shy Rose Banji wakati wa tafrija yake iliyofanyika Nyumbani Longe, Jijini Dar es Salaam.
 
Wabunge hao wa CHADEMA  ni Halima Mdee (Kawe) ambaye anaonekana pichani chini akiikataa keki hiyo iliyotolewa na wakurugenzi wa Nyumbani Longe, Bw. Gadna G Habash na mkewe Bi. Lady Jay Dee, huku mbunge wa viti Maalum, Bi. Lucy Kiwelu nae akijificha asiitazame kwa karibu.
 
Wabunge hao waliigwaya Keki hiyo kutokana na jinsi ilivyopambwa rangi za CCM.

Huku Wabunge wa CCM wakishangilia na kumtaka, Mh. Halima Mdee, aongoze ukataji wa keki hiyo ambayo ilitolewa baada ya keki ya awali iliyoandaliwa na Bi. Shy Rose kuliwa. Hata hivyo keki hiyo ilishindikana kuliwa na kuhifadhiwa.
 
Watu mbalimbali walihudhuria tafrija hiyo ndogo wakiwepo wabunge, wanasiasa, Wasanii wa muziki, watangazaji na wanahabari ambapo kila aliyesimama kuongea alimpongeza Bi. Shy Rose kwa kuwa mpambanaji katika kutafuta kile anachotaka na kumuombea kwa Mungu amuongoze vyema katika kazi yake.

Mh. Halima Mdee, Mbunge wa Kawe, akigeukia pembeni na kuonyesha ishara ya kukataa kuigusa keki ya Mh. Shy Rose Banji huku akicheka. [Chanzo: mrokim.blogspot.com]