Sunday, April 01, 2012

MAFUNZO SCHOOL OF AUTHENTIC JOURNALISM YAISHA

Mafunzo yamemalizika. Jana tulikuwa na hafla ya ufungaji. Katika picha, napokea cheti cha ushiriki toka kwa mmoja wa wakufunzi, Ivan Marovic wa Serbia. Kushoto kwangu ni Katie Halper wa Marekani. Hafla hiyo ilifanyika hapa Mexico City, kufuatia mafunzo ya uandishi wa habari, unaohusiana na masuala ya Harakati za Kijamii Zisizo na Umwagaji Damu.