Saturday, March 03, 2012

YANGA NJE LIGI YA MABINGWA AFRIKA, MATOKEO MABAYA YA NYUMBANI YAMEIMALIZA


Kocha Papic TIMU ya Yanga ya Tanzania, imeaga mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, baada ya kudungwa dozi moja bila na Zamalek ya Misri, katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Chuo cha Jeshi nchini humo jioni ya leo. Kama ilivyotarajiwa na wapenzi wa soka wa hapa nchini, Wanajangwani, walishakalia kuti kavu baada ya kuwakosa Zamalek kwenye Uwanja wa Taifa ambapo Yanga iliilazimishwa sare ya 1-1. Kwa matokeo hayo, Zamalek imeiondoa Yanga kwa jumla ya magoli 2-1.