Sunday, March 04, 2012

WAZIRI WA ELIMU AZINDUA KAMPENI YA TIGO TUCHANGE SAA 5 MPAKA 6 UNACHANGIA ELIMU KWA KUNUNUA TIGO RUSHA KWA MDA HUO

Waziri Dkt. Shukuru Kawambwa akikata utepe
Mheshimiwa
Waziri Shukuru Kawambwa,
Wawakilishi
kutoka Hassan Maajar Trust,
Wafanyakazi
wa Tigo,
Ndugu
waandishi wa habari,
Mabibi
na mabwana,

Naomba mniruhusu kuongea na nyie leo na kiswahili changu ambacho sio kizuri sana, lakini kwenye hii siku maalum ningependa nijaribu

Nina furaha kuwakaribisha wote katika siku hii nzuri ya kampeni ya Tigo Tuchange. Tuna furaha kumkaribisha Waziri wa Elimu na Ufundi Stadi, mheshimiwa Shukuru Kawambwa kama mgeni rasmi.

Tigo Tuchange ni moja ya sehemu yetu ya kusaidia jamii nchini Tanzania. Mchango wa leo unalenga kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi katika shule zenye upungufu wa vifaa, hivyo kuwawezesha kufanya vyema katika masomo yao.

Kati ya saa tano asubuhi na saa sita mchana leo, muda wa maongezi utakaonunuliwa kupitia Tigo Rusha,utaongezwa na Kampuni yetu, kwa kiwango kile kile na fedha zote zitaingia moja kwa moja kwenye kampeni.

Tulizindua Tigo Tuchange mwaka jana,na tulipata mafanikio makubwa kwani tuliweza kukusanya kiasi cha shilingi milioni ishirini na tano nukta tisa,ambazo zilitumika kununua vitabu na vifaa vingine katika shule mbalimbali nchini. Mwaka huu tunatarajia mafanikio zaidi. Hassan Maajar Trust ni moja kati ya watakaofaidika na kampeni hii,vifaa vingine vya elimu vitatolewa ambavyo vitanufaishawanafunzi wa shule za msingi.

Asanteni, na kwa pamoja tufaye mabadiliko yatakayoboresha mazingira ya wanafunzi!