Friday, March 09, 2012

SOMA, TAFAKARI, MSHTUE NA MWINGINE

MFUKO wa Afya ya Jamii(CHF), mfuko ambao unatoa huduma za matibabu kwa jamii ambayo haipo katika sekta isiyo rasmi wilayani, tarafani, katani na vijijini. Huu ni mpango wa hiari wa uchangiaji wa huduma za matibabu ya kaya/familia kabla ya kuugua.

Ni utaratibu wa hiari, unaoiwezesha kaya kupata huduma za matibabu kwa mwaka mzima kwa kuchangia kiasi cha Sh.5,000 au Sh.10,000 kwa kadiri jamii yenyewe katika halmashauri husika itakavyoamua.

Serikali kwa upande wake inachangia kwa kiwango ambacho kaya inachangia, hivyo kuufanya mfuko huu kujulikana pia kwa jina la Tele kwa Tele. Ujumbe kwa hisani ya Blogu ya Komicfirst