Sunday, March 04, 2012

SIMBA YAWAPA RAHA WATANZANIA, YAIRARUA KIYOVU

Mpikaji wa magoli ya Simba, Mganda, Emmanuel Okwi, akipanga mipango ya kumtoka mchezaji wa Kiyovu ya Rwanda katika mechi ya Kombe la Shirikisho, iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es Salaam leo. Simba imeshinda magoli 2-1, yakipachikwa na Mzambia, Felix Sunzu. 

Mashabiki wa Simba wakishangilia dozi iliyokuwa ikitolewa na Mnyama dhidi ya Kiyovu ya Rwanda kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es Salaam leo. [Picha zote: Fullshangwe Blogu]