Sunday, March 04, 2012

SIKIA HII, ETI WHITNEY HOUSTON ALIKUWA NA ‘URAFIKI’ WA SIRI NA JERMAINE JACKSON


Whitney
NI mwezi sasa imekatika tangu Nyota wa Kimarekani, Whitney Houston, kukutwa kafia bafuni kwenye hotelini moja huko Los Angeles.

Kila kukicha zimekuwa zikiibuka hadithi zikimhusisha marehemu ama familia yake. Gazeti The Sun la Uingereza, limeibuka na mpya, linadai kaka wa Michael Jackson, Jermaine Jackson, aliwahi kuwa ‘mshirika’ nyota huyo.

Gazeti hilo linadai, Jermaine,56, alishitushwa na kuumia sana baada ya kusikia kifo cha Bibie Whitney kilichotokea mwezi uliopita.

Linadai hata kibao kilichotamba cha Whitney cha ‘Saving All My Love For You’, kilikuwa maalumu kwa Jermaine.

Wakati wa uhai wake, Michael Jackson, alijua kilichokuwa kikiendelea kati ya kaka yake na ‘shemeji’ yake huyo ila hakuwahi kulisemea hilo.

Ze poziii - Whitney na Jermaine

Pamoja na kwamba walikuwa wameshamwagana kitambo, lakini inadaiwa, bado Whitney na Jermaine walikuwa washikaji na walikuwa wakitia stori vizuri tu. Hata wakati wa msiba wa Wacko, 2009, chanzo hiko kinasema, Whitney alikuwa bega kwa bega na Jermaine akimfariji kwa msiba.

Jermaine alipagawa aliposikia kifo cha Whitney, inadaiwa kutokana na maumivu aliyoyapata, ilimwia vigumu kuhudhuria mazishi aliyekuwa 'mtu wake wa karibu', Bi. Whitney Houston yaliyofanyika New Jersey.