Friday, March 09, 2012

NSSF CUP 2012 YANUKIA

Baadhi ya Wachezaji Business Times wakijifua vikali kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari Kurasini, Jijini Dar es Salaam, tayari kwa kinyang’anyiro cha Kombe la NSSF 2012, kitakachoaanza kuunguruma Jumamosi hii. Timu za soka za Jambo Leo na TBC, zitakata utepe wa mashindano hayo kwa wanaume, huku IPP Media wakitarajia kuumana na Mwananchi katika mchezo wa netiboli.

Wachezaji wa Business Times, Mweta(bukta nyekundu), Victor Mkumbo(bluu) na Ibra Kitala(jezi nyeupe), wakiwa mazoezini kama walivyokutwa na Blogu hii kwenye Viwanja vya Shule ya Sekondari Kurasini, Jijini Dar es Salaam, jana.