Saturday, March 03, 2012

Mchezaji hatari wa Mburahati Queens na Timu ya Taifa ya Wanawake, Twiga, Mwanahamis Omary(8), akipewa tano na wachezaji wenzake baada ya kuifungia goli timu yake dhidi ya Sayari katika mechi ya Ligi ya Wanawake Mkoa wa Dar es Salaam iliyoanza kuunguruma leo kwenye Uwanja wa Karume, Jijini Dar es Salaam leo. Mburahati Queens imeigalagaza bila huruma Sayari, magoli 7-0. Ligi hiyo inaendelea kesho hapo hapo Karume kwa kuzikutanisha timu za Evergreen na Temeke Queens zote za Temeke. Mchezo huo utachezwa saa 7.30 mchana.