Sunday, March 04, 2012

MATUKIO MBALIMBALI YA UFUNGAJI WA LIGI YA NETIBOLI JANA

Timu zikipita mbele ya mgeni wa rasmi, Mh. Dkt. Mary Mwanjelwa, Mbunge(hayupo) pichani, zikiashiria kwisha kwa Ligi ya Netiboli Taifa, iliyokuwa ikiunguruma kwenye Viwanja vya Sigara Jijini Dar es Salaam, ambapo  Bandari Dar es Salaam, imenyakuwa ubingwa wa michuano hiyo.
ALIYETESA: Mgeni wa rasmi, Mh. Dkt. Mary Mwanjelwa, Mbunge, akimkabidi Matalena Mhagama zawadi yake baada ya kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa mashindano hayo. Wengine katika picha, kutoka kushoto, Mke wa Katibu Mkuu CCM, Mama Mkama, Mh. Idd Azan, Mbunge wa Kinondoni na Mh. Abas Mtemvu, Mbunge wa Temeke.


ALIWASHIKA: Sharifa Mustafa akifurahia kombe lake baada ya kuibuka kuwa mzuiaji makini wa ligi hiyo.

SHUTA ALIYETISHA: Nasra Selemen akipeana mkono na Mgeni rasmi, Mh. Dkt. Mary Mwanjelwa, mara baada ya kupewa zawadi yake ya 'shuta' bora.

NIDHAMU MICHEZONI: Mchezaji wa Timu ya Umoja Queens ya Pwani, akipokea zawadi ya timu yenye nidhamu kwa niaba ya kikosi chake.


FULL SHANGWE: Mabingwa wa Netiboli Ligi Daraja la Pili Taifa, Bandari Dar es Salaam katika picha ya pamoja na Mgeni Rasmi, Mh. Dkt. MAry Mwanjelwa.

NYOTA WA BAADAE: Mtoto aliyejitambulisha kwa jina moja la Kulwa, akifuatilia kwa makini shamrashamra hizo.