Friday, March 02, 2012

'LILIAN INTERNET' ABWAGA MANYANGA TWANGA PEPETA , ATIMKIA MASHUJAA


Lilian
BENDI ya muziki wa dansi, Mashujaa Musica, imeendelea kuioneshea ushujaa bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’, safari hii ikimnyakuwa mnenguaji wake mahiri, Lilian Tungarazal almaarufu  ‘Intanet’ .

Meneja wa Mashujaa, Maximilian Luhanga, alisema kwamba wameamua kumchukua mwanamuziki huyo ili kuimarisha bendi yao na tayari wameshasaini mkataba wa miaka miwili na ‘kifaa’ hiko. Alisema onesho la utambulisho linatarajiwa kufanyika Jumatano ijayo katika Ukumbi wa Nyumbani Lounge, Jijini Dar es Salaam.

 Hii ni mara ya pili kwa Mashujaa kuibomoa Twanga Pepeta. Mapema mwaka huu ilimyakua mwaimbaji mahiri, Charlz Gabriel ‘Chaz Baba’.