Saturday, March 03, 2012

LIGI NETIBOLI DARAJA LA PILI TAIFA YAMALIZIKA LEO, BANDARI DAR WATWAA UMALKIA

Mgeni rasmi, Mh. Dkt. Mary Mwanjelwa(Mbunge), akimkabidhi kombe la ubingwa wa Ligi ya Netiboli Daraja la Pili Taifa, nahodha wa timu ya Bandari Dar es Salaam, Judith Ilunda kwenye Viwanja vya Sigara, Jijini Dar es Salaam leo. Bandari wametwaa umalkia huo baada ya kuzoa juimla ya pionti 14.

Wachezaji wa Timu ya Tumaini ya Dar es Salaam (rangi nyekundu), wakipambana na akina dada wa Temeke Queens, katika mechi ya mwisho ya Ligi Netiboli Daraja la Pili iliyochezwa kwenye Viwanja vya Sigara Jijini, Dar es Salaam leo. Tumaini imeichapa Temeke Queens magoli 22-19. Picha zaidi za shamra shamra za ufungaji ligi hiyo ziko njiani.