Thursday, March 01, 2012

BANDARI DAR YAENDELEA KUTOA DOZI LIGI YA NETIBOLI

Mchezaji mkongwe wa timu ya Bandari Dar es Salaam, Nuru Fundi(WA), akimtoka Agnes Yohane(WD) wa Kambangwa pia ya Dar es Salam, katika mchezo safi wa Ligi ya netiboli daraja La pili Taifa, uliopigwa jioni hii kwenye Viwanja vya Sigara, Jijini Dar es Salaam. Bandari imeikamua Kambangwa bila huruma magoli 48-18.

Mchezaji wa timu ya Temeke Queens, Naima Ramadhan(GS), akijaribu kumuadaa mpinzani wake wakati wa mchezo baina yao na timu ya Kurugenzi katika mechi ya Ligi ya netiboli daraja la pili Taifa, uliofanyika kwenye Viwanja vya Sigara, Jijini Dar es Salaam, jioni hii. Temeke Queens, ilishinda magoli 31-28. Picha na matokeo zaidi ya michezo iliyopigwa leo badae kidooogo.