Saturday, February 18, 2012

WAWAKILISHI WETU TUPENI RAHA LEO

Klabu kongwe nchini, Yanga na Simba, leo zinajimwaga dimbani, Yanga ikiikaribisha Zamalek ya Misri Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam hapo Jumamosi kwa pambano mchezo wa raundi ya awali ya CAF wakati huo huo, Simba wakicheza ugenini huko Kigali, Rwanda na Kiyovu kwenye Kombe la Shirikisho.

Mbali ya wakongwe hawa, Timu za Zanzibar, Mafunzo na Jamhuri, nazo zitaingia uwanjani kwa Mafunzo kucheza na Liga Muculmana de Maputo ya Msumbiji kwenye kombe la washindi la CAF  na Jamhuri kuivaa Hangwe ya Zimbabwe kwenye Kombe la Shirikisho.

Yanga
Tayari Zamalek, (mabingwa wa Afrika mara 5) wameshatua Dar es Salaam bila nyota wake, Ahmed Hassan, Muhammad Ibrahim na Salah Suleiman. Hivi karibuni, Zamalek walicheza mechi yao ya mwisho ya majaribio na kuifunga Telecom Egypt bao 4-1 kwa bao za Amr Zaki, Ibrahim Hassan na Ahmad Jaffar.


Simba yaenda Rwanda bila Wachezaji kadhaa

Simba iliondoka Alhamisi jioni kwenda Kigali, Rwanda kupambana na Kiyovu huku ikiacha nyuma kadhaa wakiachwa. Wachezaji hao ni pamoja na Gervais Kargo, Derrick Walulya, Haruna Moshi 'Boban', Ulimboka Mwakingwe, Amir Maftah na Hassan Khatib na imesemwa baadhi yao ni majeruhi.

Pamoja na Kocha Cirkovic Milovan na Wasaidizi wake Amatre, Daktari Cosmas Kapinga na James Kisaka, Kocha wa Makipa, Viongozi wengine ambao wamo kwenye msafara huo ni Makamu Mwenyekiti Geofrey Nyange 'Kaburu', Katibu mkuu Evodius Mtawala, Fransis Silaya (Mjumbe wa Kamati ya Utendaji).

Wachezaji waliosafiri ni:
Makipa: Juma Kaseja na Ali Mustapha 'Barthez'. Mabeki: Nassor Said 'Cholo', Juma Jabu, Juma Nyoso, Kelvin Yondan, Victor Costa na Obadia Mungusa. Viungo: Shomari Kapombe, Mwinyi Kazimoto, Jonas Mkude na Patric Mafisango Washambuliaji: Ramadhani Singano 'Messi', Edward Christopher, Salum Machaku, Uhuru Selemani, Felix Sunzu na Emmanuel Okwi.

Blogu hii inawatakia kila la heri wawakilishi wetu. Pamoja!