Wednesday, February 22, 2012

WABAKA MTOTO WA MIAKA 11, WACHUKUA PICHA ZA VIDEO. JAJI AONA SIO ISHU KIVIIILE, AWAFUNGA MIEZI 40


WAHENGA walisema, tembea uone. Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Jaji, David Farrell QC, wamewaacha mashuhuda waliokuwa kwenye mahakama ya Luton Crown midomo wazi, baada ya kuwahukumu masela, Roshane Channer na Ruben Monteiro wenye umri wa 21 kila mmoja, jumla ya miezi 40, sawa na miaka mitatu kwa kosa la kumbaka binti wa miaka 11.

‘Pamoja na kuwa na umri mdogo, lakini ushahidi unaonesha kuwa,  binti alikubali ‘zoezi’ hilo kwa roho safi’, alisema Jaji Farrell.

Jaji Farrell: Binti 'alifurahia' kubakwa
Mkurugenzi wa Rape Crisis charity, Bi. Yvonne Traynor, alinukuliwa akisema: ‘Hii ni hukumu ‘kituko’ ambayo sijawahi kuona. Kwa akili ya kawaida ambayo haiitaji shule, haiingii akilini, mtoto wa miaka 11 akubali kuingiliwa na vidume viwili kwa wakati mmoja tena huku mwingine akiwapiga picha’, alisema Bi. Traynor.

‘Hivi Jaji anaelewa kuwa motto wa umri huo huwa hawezi kuamua jambo na pia atakuwa ameathirika kisaikolojia? Wakati umefika sasa, mahakama kuwalinda wanawake na wasichana dhidi ya wabakaji’, alisema Bi. Traynor?

Wehu, Channer na Monteiro wanadaiwa kufanya tukio hilo Julai mwaka jana ghorofani, kwenye mitaa ya Luton.

Jaji Farrell alisema: ‘Ushahidi unaonesha kuwa, mbakwaji ‘hakuonewa’ kwenye mkasa huo, isitoshe watuhumiwa walikubali kutenda kosa hilo toka mwanzo wa kesi’.

Lakini akasema: ‘Ila ni kweli kuwa Channer na Monteiro walikuwa na nia mbaya ya kumdhalilisha ‘mpenzi’ wao kwa faida yao kwani wakati wa tukio hilo, walikuwa wakichukua picha za video’.

Aliongeza kuwa: ‘Kuna ushahidi kuwa video hiyo imesambaa na pia ilikutwa kwa mmoja wa ‘vichaa’ hao.

Nao, Shy Keenan na Sara Payne, ambao mtoto wao, Sarah, akiwa na miaka nane aliuawa mwaka 2000 na Roy Whiting, wakizungumzia hukumu hiyo walisema: ‘Kifungo walichopewa hawa vijana ni kiduchu mno, hilo halina ubishi’.

‘Jamani, Mtoto wa miaka 11anachukuliwa kama wa miaka 14, wakati hata hakufikisha miaka 18! Tutakata rufaa kwa Mwanasheria Mkuu. Ni muda mrefu sasa umepita hatujalalamikia maamuzi ya aina hii yasiyovumilika’ wamesema waathirika hao. [Chanzo: Mashirika]